CCM Pwani yawataka vijana kutumia fursa za mikopo

Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani, Musa Mansur, amewataka vijana kutunza tunu ya amani nchini na kuepuka kujiunga na makundi yasiyofaa yanayoweza kuhatarisha usalama na mshikamano wa jamii.

‎Mansur ametoa wito huo Agosti 7, 2026, muda mfupi baada ya kufungua Baraza la Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Kibaha Mjini, lililofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere, Kwamfipa.

‎Amesema vijana wanapaswa kuwa wamoja, kushikamana na kufuata kanuni, taratibu na misingi ya Chama katika kutatua changamoto zinazowakabili, akisisitiza kuwa wao ni sehemu muhimu ya kulinda amani na mshikamano wa Taifa.

‎ “Vijana wanatakiwa kushikamana kwani wao ndio moyo wa Chama. Pendaneni na mkiona kuna changamoto, tafuteni namna ya kuitatua kwa kufuata kanuni za Chama,” amesema Mansur.

‎Aidha, Mansur amewahimiza vijana kujiunga katika vikundi vya uzalishaji na kujishughulisha na shughuli za kiuchumi ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali, ikiwemo mikopo inayotolewa kwa ajili ya kuwawezesha kiuchumi.

Post a Comment

Previous Post Next Post