Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha, Cecilia Daniel Paresso, amewataka wanawake nchini kutumia fursa mbalimbali zinazopatikana katika halmashauri zao ili kujenga uwezo wa kiuchumi na kuboresha maisha yao.
Paresso ametoa wito huo wakati akizungumza na wanachama wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Meru mkoani Arusha, ambapo amewahimiza wanawake kuwa mstari wa mbele katika kuchangamkia fursa za maendeleo zinazotolewa na Serikali, ikiwemo mikopo inayotolewa na halmashauri kwa ajili ya kuwawezesha kiuchumi.
Amesema wanawake wanapaswa kutumia fursa hizo kwa ufanisi kwa kuanzisha na kuendeleza shughuli mbalimbali za uzalishaji ili kuongeza kipato cha familia na kushiriki kikamilifu katika ukuaji wa uchumi wa taifa.
“Wanawake tunapaswa kuwa chachu ya maendeleo katika maeneo yetu kwa kutumia fursa zilizopo, ikiwemo mikopo ya halmashauri, ili kujenga msingi imara wa kiuchumi na kuinua maisha yetu,” amesema Paresso.

Post a Comment