Mtangazaji maarufu wa masuala ya siasa nchini, Chief Odemba, amehitimu mafunzo ya siasa na uongozi kwa vijana yaliyofanyika nchini Marekani kupitia mpango wa kimataifa wa International Visitor Leadership Program (IVLP) unaoratibiwa na Serikali ya Marekani.
Mafunzo hayo yaliwakutanisha vijana viongozi pamoja na wataalamu kutoka mataifa mbalimbali duniani kwa lengo la kubadilishana uzoefu, kujifunza mbinu bora za uongozi, pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika masuala ya uongozi na maendeleo.
Katika kipindi chake cha mafunzo nchini Marekani, Chief Odemba alipata fursa ya kutembelea taasisi mbalimbali muhimu ikiwemo Seneti ya Marekani iliyopo Washington, D.C., ambako alishiriki mijadala kuhusu masuala ya demokrasia, utawala bora, maendeleo ya vijana, ushiriki wa wananchi katika maamuzi na nafasi ya viongozi vijana katika kujenga jamii zenye uwajibikaji.

Post a Comment