Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dkt. Dorothy Gwajima, ameitaka Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru iliyopo mkoani Arusha kuhakikisha inawaandaa wahitimu wake kwa kuwapa ujuzi unaowawezesha kujiajiri na kuanzisha shughuli za kiuchumi badala ya kutegemea ajira za kuajiriwa pekee.
Dkt. Gwajima ameyasema hayo wakati akizindua Bodi ya Uendeshaji ya taasisi hiyo, ambapo amesisitiza umuhimu wa kubadilisha mtazamo miongoni mwa wanafunzi na wahitimu ili waweze kuona elimu wanayoipata kama nyenzo ya kutengeneza fursa za maendeleo binafsi na kwa jamii kwa ujumla.
Amesema kuwa katika mazingira ya sasa, elimu inapaswa kwenda sambamba na ujuzi wa vitendo unaomwezesha mhitimu kutambua changamoto zilizopo katika jamii na kuzigeuza kuwa fursa za kiuchumi.
“Ni muhimu wahitimu wetu wasisubiri ajira pekee, bali wawe wabunifu, waweze kutumia taaluma zao kuanzisha miradi mbalimbali itakayowapatia kipato na pia kutoa ajira kwa wengine,” amesema Dkt. Gwajima.

Post a Comment