Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, amesema uongozi wa chama hicho utaweka utaratibu maalumu wa kupata msimamo wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, kufuatia kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kuhusu moja ya vyama vya siasa ambavyo bado vinaendelea kujitafakari iwapo vitashiriki katika mazungumzo ya maridhiano.
Akizungumza kuhusu suala hilo, Mnyika amesema kuwa Tundu Lissu ndiye Mwenyekiti halali wa CHADEMA na kwa kuwa kwa sasa anashikiliwa gerezani, ni muhimu chama kufuata utaratibu rasmi wa kupata maoni na msimamo wake kabla ya kufikia uamuzi wowote unaohusu ushiriki wa chama katika mazungumzo hayo.
Ameeleza kuwa uongozi wa CHADEMA unaona ni wajibu kuhakikisha maamuzi ya chama yanafanyika kwa kuzingatia uongozi uliopo pamoja na taratibu za chama, hivyo hatua ya kwanza ni kuhakikisha msimamo wa Mwenyekiti unafahamika kabla ya kutangaza uamuzi wowote rasmi. SOMA ZAIDI.
Post a Comment