Mnyika avunja ukimya kuhusu Mwenendo wa kesi ya Lissu, atoa wito huu mkubwa kwa watanzania

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, ametoa wito kwa viongozi, wanachama, wafuasi wa chama hicho pamoja na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, kuanzia Agosti 10, 2026, kufuatilia mwenendo wa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Jumatatu, Agosti 3, 2026, Mnyika amesema kesi hiyo inatarajiwa kuendelea kusikilizwa baada ya kusimama kwa kipindi fulani kutokana na hatua za kisheria zilizochukuliwa katika Mahakama ya Rufani.

Kwa mujibu wa Mnyika, kusimama kwa mwenendo wa kesi hiyo kulitokana na rufaa iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), ambaye alikuwa akipinga uamuzi wa Mahakama Kuu wa kutokubali kupokea ushahidi wa ziada uliowasilishwa na upande wa mashtaka.

Amesema ushahidi huo ulihusisha maelezo ya aliyekuwa Mpelelezi Mkuu wa matukio yaliyotokea nchini Oktoba 29, 2025, siku ya Uchaguzi Mkuu, pamoja na siku zilizofuata, ambaye ni ACP Amin Mahamba. SOMA ZAIDI

Post a Comment

Previous Post Next Post