Nchimbi Ang'oa Kofia Kuhusu Sababu Za Lissu Kusota Gerezani

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Emmanuel Nchimbi, amesema kile alichokiita "vikesi vya kijinga kijinga" ndicho kilichochangia Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, kuendelea kusota gerezani kwa takribani mwaka mmoja, akihusisha hali hiyo na mfumo wa sheria na Katiba ya sasa.

Kauli hiyo ilitolewa na Nchimbi hivi karibuni, ambapo alieleza kuwa hali ya Lissu kuendelea kuwa gerezani kwa muda mrefu imetokana na mfumo wa sheria na Katiba ambao, kwa mtazamo wake, unaruhusu haki kucheleweshwa na kuwafanya baadhi ya viongozi kuwa juu ya sheria badala ya kuwajibika sawa na wananchi wengine.

Akifafanua zaidi msimamo wake, Makamu wa Rais alieleza kuwa changamoto hiyo ya kucheleweshwa kwa haki inatokana na mapungufu yaliyopo ndani ya mfumo wa kisheria na kikatiba wa sasa, akisisitiza kuwa mfumo huo unahitaji marekebisho ya kina ili kuhakikisha haki inatendeka kwa wakati kwa wote bila kujali nafasi zao za kisiasa au kijamii. SOMA ZAIDI.


Post a Comment

Previous Post Next Post