Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA Taifa (BAVICHA), Wakili Deogratias Mahinyila, amemjibu Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, kufuatia kauli yake ya kuwataka Watanzania kuendelea kupigania kupatikana kwa Katiba Mpya.
Akizungumza Julai 24, 2026, Mahinyila alisema kuwa, kwa mtazamo wake, watu wengi waliojitokeza hadharani kudai Katiba Mpya wamejikuta wakikabiliwa na changamoto mbalimbali za kisheria, ikiwemo kufunguliwa mashitaka ya ugaidi na uhaini.
Mahinyila alimtaja Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Tundu Lissu, pamoja na baadhi ya vijana wa CHASO wanaoshikiliwa kwa tuhuma za ugaidi, akidai kuwa walikuwa wakitetea ajenda ya Katiba Mpya kabla ya kukamatwa na kufikishwa mahakamani.
Kwa mujibu wa Mahinyila, hali hiyo imekuwa ikituma ujumbe wa hofu kwa wananchi wanaotamani kushiriki katika mjadala wa mageuzi ya kisiasa na mchakato wa kupata Katiba Mpya yenye maridhiano ya wadau mbalimbali. SOMA ZAIDI.
Post a Comment