Nyumbani Kwa Askari Aliyestaafu Mwaka 1976 Askari Wenzake Wamtembelea

Nyumbani kwa askari aliyestaafu mwaka 1976 askari wenzake wamtembelea

Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji wameonyesha mfano wa mshikamano na kuthamini mchango wa watumishi waliostaafu baada ya kumtembelea askari mstaafu WP 936 PC Zainabu Salumu nyumbani kwake katika kitongoji cha Nyampaku, Kijiji cha Muhoro, wilayani Rufiji mkoani Pwani. 

Ziara hiyo iliongozwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Rufiji, SACP Protas Mutayoba, akiongozana na askari wa vyeo mbalimbali kwa lengo la kumjulia hali mstaafu huyo na kufahamu changamoto anazokabiliana nazo katika maisha yake ya kila siku.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Kamanda Mutayoba alisema kuwa Jeshi la Polisi lina utaratibu wa kuendelea kuwajali askari waliostaafu kwa kutambua mchango wao mkubwa walioutoa walipokuwa kazini. 

Alieleza kuwa lengo la kuwatembelea wastaafu ni kuwapa faraja, kusikiliza mahitaji yao na kutafuta namna ya kuyapatia ufumbuzi pale inapowezekana. SOMA ZAIDI.


Post a Comment

Previous Post Next Post