Msemaji wa Jeshi la Iran, Jenerali Abolfazl Shekarchi, amedai kuwa Marekani imetumia silaha ambazo hazijawahi kutumika duniani katika operesheni zake za kijeshi dhidi ya Iran.
Silaha zinazotumiwa na Marekani dhidi yetu ni katika zile akiba ambazo Serikali ya Marekani ilipanga kutumika kama silaha za mashambulizi kama vitatokea vita vya tatu vya dunia.
Shekarchi amesema hatua hiyo inaonesha kiwango cha juu cha mashambulizi yanayoendelea kufanywa na Washington dhidi ya Tehran, huku akisisitiza kuwa Iran itaendelea kujibu kile ilichokiita uchokozi wa Marekani.
Kauli hiyo imekuja wakati Marekani ikiendelea na mashambulizi dhidi ya malengo mbalimbali ndani ya Iran, huku Tehran nayo ikijibu kwa kushambulia nchi washirika wa Washington katika eneo la Ghuba.

Post a Comment