Jeshi la Ukraine limeshambulia meli ya Urusi iliyobeba silaha kuelekea Iran- Zelensky

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametangaza kuwa jeshi la nchi yake limefanya mashambulizi dhidi ya meli za Urusi katika bahari ya Kaspia, hatua ambayo imeibua mjadala mkubwa wa kimataifa kuhusu upanuzi wa vita nje ya mipaka ya kawaida ya Ukraine. 

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari vya kimataifa, Zelensky amesema meli hizo za Urusi zilikuwa zikisafirisha vifaa vya kijeshi vinavyotoka Iran, ikiwemo droni na silaha zinazotumika katika mashambulizi dhidi ya Ukraine.

Post a Comment

Previous Post Next Post