Mvutano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Urusi umeendelea kuvuta hisia baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutoa onyo kali kuhusu uwezekano wa Russia kuendelea kushirikiana na Iran katika masuala ya kijeshi.
Kauli hizo zimekuja wakati hali ya usalama Mashariki ya Kati ikiendelea kuwa tete, huku mataifa makubwa yakifuatilia kwa karibu mwenendo wa mgogoro huo.
Trump amesema hadharani kuwa hataki kuona Russia au China zikiiunga mkono Iran kwa silaha, akisisitiza kuwa hatua kama hiyo inaweza kuathiri uhusiano wa Washington na mataifa hayo.
Trump amesema hadharani kuwa hataki kuona Russia au China zikiiunga mkono Iran kwa silaha, akisisitiza kuwa hatua kama hiyo inaweza kuathiri uhusiano wa Washington na mataifa hayo.
Pia ameashiria uwezekano wa kutumia hatua za kiuchumi, ikiwemo ushuru mkubwa wa bidhaa, endapo kutakuwa na ushahidi wa ushirikiano unaokwenda kinyume na msimamo wa Marekani. SOMA ZAIDI.
Post a Comment