Tafadhali Zingatia: Ikiwa unasoma kwenye PHOENIX, tafadhali bofya kitufe cha “Soma Makala Asili” kilicho upande wa juu kulia ili kusoma makala kamili.
Kijana mmoja anayedaiwa kuhusishwa na vitendo vya wizi katika Mtaa wa Makao Mapya mkoani Arusha ametoweka baada ya wananchi kudai kukuta vitu mbalimbali vinavyoshukiwa kuwa mali za wizi ndani ya nyumba aliyokuwa akiishi.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wakazi wa eneo hilo, tukio hilo lilibainika baada ya wananchi kupata taarifa kuhusu uwepo wa mali zinazohisiwa kuibwa katika nyumba ya kijana huyo. Baada ya kufika eneo husika na kufanya uchunguzi wa awali, wananchi walidai kukuta vitu mbalimbali ikiwemo magodoro matano pamoja na mtungi wa gesi.
Wananchi hao walisema baadhi ya mali zilizokutwa zilitambuliwa na wakazi wa mtaa huo kuwa ni vitu vilivyokuwa vimeripotiwa kupotea katika nyakati tofauti. Hali hiyo ilizua taharuki na mjadala mkubwa miongoni mwa wakazi wa eneo hilo ambao kwa muda wamekuwa wakilalamikia matukio ya wizi yanayojitokeza mara kwa mara.Endelea Kusoma Kwa Kubofya Hapa.

Post a Comment