Tafadhali Zingatia: Ikiwa unasoma kwenye PHOENIX, tafadhali bofya kitufe cha “Soma Makala Asili” kilicho upande wa juu kulia ili kusoma makala kamili.
Wananchi wa Kijiji cha Chang’ombe, Kata ya Ndevelwa, wilaya na mkoa wa Tabora wameungana na kumuua nyoka mkubwa aina ya Sawaka mwenye urefu wa zaidi ya futi 12 baada ya msako uliochukua zaidi ya saa kumi.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo hilo, nyoka huyo amekuwa akidaiwa kusababisha hofu kwa wakazi wa kijiji hicho kwa muda wa zaidi ya miaka minne, akihusishwa na kumeza mifugo ikiwemo kuku, mbuzi na mbwa.
Tukio hilo limechukua mkondo mpya baada ya nyoka huyo kudaiwa kumvamia mwanamke mmoja, tukio ambalo liliibua hasira na hofu kwa wananchi, hali iliyosababisha kuanzishwa kwa msako mkubwa wa kumtafuta.
Wananchi wamesema walilazimika kushirikiana kwa pamoja ili kumdhibiti mnyama huyo hatari ambaye alikuwa akihatarisha maisha yao na mali zao kwa muda mrefu.Endelea Kusoma Kwa Kubofya Hapa.
Post a Comment